Mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia,Jhonier Blanco ataitumikia klabu ya KMC kwa mkopo wa msimu mzima wa 2025/26 akitokea klab ya Azam
Kocha wa KMC Mbrazil Marcio Maximo anaenda kupata huduma ya nyota huyu ambaye wanatoka bara moja la Amerika ya Kusini
KMC tayari imekamilisha mchakato wa kumsajili mshambuliaji huyo na wakati wowote watamtambulisha
Blanco ameitumikia Azam Fc msimu uliopita lakini alikuwa na nafasi finyu ya kuanza katika kikosi cha kwanza
Kocha mpya Florente Ibenge nae ameonekana kutomuhitaji baada ya Azam Fc kumsajili mshambuliaji kutoka DR Congo Japhet Kitambala