Stars yaifuata Congo, kufuzu kombe la Dunia

Joel JJ By Joel JJ β€’ 3rd September 2025


Stars yaifuata Congo, kufuzu kombe la Dunia

Kikosi cha Timu ya Taifa 'Taifa Stars' kimeondoka nchini Alfajiri ya hii leo kwenda nchini Congo Brazzaville tayari kwa mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Congo Brazzaville.

Mchezo huo utapigwa Septemba 5, 2025 kwenye Uwanja wa Alphonse Massemba-Debat kuanzia saa 1:00 Usiku.

Stars ipo kundi E, ikishika nafasi ya pili ikiwa na pointi 9 katika mechi 5, ikiongozwa na Morocco yenye pointi 15, Zambia nafasi ya tatu pointi 6 sawa na Niger iliyopo nafasi ya 4 huku Congo Brazzaville ikishika mkia ikiwa na pointi 0 katika mechi tano ilizocheza.

Baada ya mchezo huo, Stars itarejea Tanzania kuumana na Niger katika mchezo utakaopigwa Jumanne Septemba 09 dimba la New Amaan Complex, Zanzibar


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.