Klabu ya Simba leo imemtambulisha beki wake mpya Wilson Nangu anayetua kutoka klabu ya JKT Tanzania
Simba imekamilisha usajili wa beki huyo ambaye pia amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars' kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Congo na Niger
Nangu amesaini mkataba wa miaka mitatu kuwatumikia Wekundu hao wa Msimbazi





