International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano Oktoba 15 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Oct 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano Oktoba 15 2025

Klabu ya Italia Inter Milan imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa kati wa Crystal Palace Marc Guehi lakini Liverpool bado wanapewa nafasi kubwa ya kuinasa saini ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 25. (Tuttosport - In Itali)

Mshambulizi wa Bournemouth Antoine Semenyo ana kipengele cha kuachiliwa huru katika kandarasi yake lakini Cherries wanaficha hilo kwa sababu wanataka kusalia na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana mwenye umri wa miaka 25 ambaye amekuwa akihusishwa na Tottenham na Manchester United. (Sportsport)

Chelsea na Barcelona wanamfuatilia mshambuliaji wa Dinamo Zagreb Mreno Cardoso Varela, 16. (Mundo Deportivo - In Spanish)

Brighton hawana mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Cameroon Carlos Baleba mwezi Januari licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kuvutiwa na Manchester United msimu uliopita. (Sportsport)

Manchester United wamemweka kiungo wa kati wa Crystal Palace na England Adam Wharton, 21, juu ya Baleba kwenye orodha ya wachezaji inaowalenga ili kuhamia timu hiyo. (Subscription Required)

Manchester United wanafikiria kuongeza mkataba wa kiungo wa kati wa Brazil Casemiro zaidi ya msimu huu, lakini tu ikiwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 atakubali kupunguziwa mshahara. (Mail)

Kumekuwa na nia ya kumnunua Casemiro huko Brazil na Saudi Arabia lakini kocha wa Manchester United Ruben Amorim anaweza kuwasilisha hoja ya mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid asalie. (ESPN)

Mlinda lango wa Barcelona Marc-Andre ter Stegen, 33, ameweka wazi kuwa hana mpango wa kuondoka katika klabu hiyo licha ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani kuvutia vilabu vikiwemo Manchester United na Newcastle United. (Diario AS - In Spanish)

Beki wa Crystal Palace Daniel Munoz anasakwa na Barcelona lakini The Eagles hawatamruhusu mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia mwenye umri wa miaka 29 kuondoka mwezi Januari. (Fichajes - In Spanish)

Uamuzi wa aliyekuwa afisa mkuu wa kandanda wa Tottenham Scott Munn kuchukua nafasi katika klabu ya Parma ya Italia badala ya Nottingham Forest ni dalili zaidi kwamba kocha Ange Postecoglou yuko katika mazingira ya kupoteza kazi yake. (Sportsport)

Mkurugenzi mpya wa michezo wa Newcastle Ross Wilson ataongoza ukaguzi wa hali ya kandarasi ya wachezaji wakuu wa klabu hiyo huku klabu hiyo ikitarajia kumaliza marudio ya sakata ya uhamisho ambayo ilimfanya mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 26, kujiunga na Liverpool. (Subscription Required).

Chelsea hawana wasiwasi wowote kuhusu mustakabali wa kiungo wa Ecuador Moises Caicedo, 23, kufuatia ajenti wake kuadhibiwa hadharani. (Telegraph - Subscription Required)

Caicedo anatarajiwa kutuzwa kandarasi mpya na Chelsea ili kuzuia nia ya Real Madrid. (TeamTalks)

Borussia Dortmund wanavutiwa na kiungo wa kati wa Barcelona na Uhispania Guille Fernandez mwenye umri wa miaka 17 ambaye bado hajacheza katika kikosi cha kwanza katika klabu hiyo ya Catalan. (Bild - In Deutch)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’