Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) jana imefungwa 2-0 na Iran kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopigwa katika uwanja wa Rashid, Dubai.
Stars imepoteza mechi zake tatu mfululizo kwenye michuano yote huku ikishindwa kupata ushindi kwenye mechi 6 mfululizo vipigo vinne, sare mbili.
Ilipoteza mechi mbili za mwisho kuwania kufuzu kombe la Dunia ikifungwa 1-0 na Zambia na Niger
Akizungumza baada ya mchezo wa jana, kocha Hemed Suleiman 'Morocco' alisema alitumia mchezo huo kuwapa nafasi wachezaji zaidi ikiwa ni katika mpango mkakati wa kuunda kikosi imara kwa ajili ya michuano ya Afcon itakayofanyika baadae mwaka huu nchini Morocco