International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Oktoba 17 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
17 Oct 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Oktoba 17 2025

Manchester United wangetaka takriban pauni milioni 40 kumruhusu nahodha wao Bruno Fernandes, 31, kuondoka na kujiunga na klabu nyingine ya Ulaya, huku Bayern Munich wakihusishwa pakubwa na kutaka kumnunua kiungo huyo wa kati wa Ureno. Team Talks)

Liverpool wanatazamia uhamisho wa euro 90m (Β£78m) kwa mshambuliaji wa Uhispania na Athletic Club Nico Williams, 23. (Fichajes - In Spanish)

Liverpool pia wanatarajiwa kutafuta saini ya beki wa Borussia Dortmund na Ujerumani Nico Schlotterbeck, 25, kuhusu uhamisho wa majira ya joto. (Sports Illustrated)

Barcelona wanafikiria kumnunua fowadi wa Juventus na Serbia Dusan Vlahovic, 25, ambaye atakuwa mchezaji huru msimu ujao. (AS - In Spanish)

Bayern Munich pia wanasemekana kuwania saini ya Vlahovic, huku miamba hao wa Ujerumani wakihofia kuwa klabu nyingine inaweza kuanzisha kipengele cha kumnunua mshambuliaji wa Uingereza, Harry Kane, 32, kutoka kwao. (Mirror)

Mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Elliot Anderson, 22, ana uhakika atajumuishwa kwenye orodha ndefu ya wachezaji wanaolengwa na Newcastle msimu wa joto, ambao wana nia ya kumrejesha kiungo huyo wa Nottingham Forest Kaskazini Mashariki. (Mail - Subscription Required)

Real Madrid wanamfuatilia kwa karibu mlinzi wa Bayern Munich Dayot Upamecano, 26, huku mkataba wake wa kimataifa na Ufaransa ukikamilika msimu ujao na yuko tayari kusikiliza ofa zingine. (Fichajes - Spanish)

Real Madrid wanaweza kumpeleka Endrick, 19, kwa mkopo mwezi Januari, lakini West Ham haionekani kuwa mahali pazuri kwa fowadi huyo wa Brazil. (TeamTalks)

Real Madrid pia wanajiandaa kupata ofa kwa fowadi Gonzalo Garcia mwezi Januari. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alionyesha kiwango kizuri cha mchezo kwenye Kombe la Dunia la Klabu ya Fifa, lakini asasa kiwango chake kimeshuka . (Marca - In Spanish)

Barcelona wanamtazama fowadi wa Hoffenheim na Kosovo Fisnik Asllani, 23, ambaye anaweza kuondoka katika klabu hiyo ya Ujerumani msimu ujao wa joto. (Sky Germany)

Kiungo wa kati wa Red Bull Salzburg, 20, Bobby Clark, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo kwenye Championship Derby, anatarajiwa kuhama Januari hadi mabingwa wa Ligi Kuu ya Uskoti Celtic. (Times - Subscription Required)

BBC

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
8h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
11h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
13h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
15h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
17h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
18h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
18h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
20h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
23h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’