Kikosi cha Simba kimewasili salama Tunis huko Tunisia kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Esperance utakaopigwa Jumamosi.
Simba iliondoka nchini mapema leo ikipitia Istanbul, Uturuki.
Hata hivyo Simba imekabiliwa na ucheleweshwaji uwanja wa ndege kwa saa kadhaa kutokana na taratibu walizokutana nazo.




