Local,Normal News,Yanga, Ahly

Yanga yapoteza ugenini dhidi ya Al Ahly

Joel JJ By Joel JJ
β€’
23 Jan 2026
Yanga yapoteza ugenini dhidi ya Al Ahly

Mabao mawili ya Trezeguet yameihakikishia Al Ahly ushindi muhimu wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa ligi ya mabingwa uliopigwa uwanja wa Borg El Arab huko Misri.

Yanga ilicheza kwa nidhamu kubwa kipindi cha kwanza lakini walipoteza umakini dakika za lala salama kipindi cha kwanza Trezeguet akifunga bao la uongozi kwa kichwa.

Kipindi cha pili kocha wa Yanga Pedro Goncalves alifanya mabadiliko kidogo ya kimbinu akiwaingiza Mudathir Yahya na Pacome Zouzoua akijaribu kusaka bao la kusawazisha.

Hata hivyo kupotea kwa umakini eneo la kati ya uwanja kukawanufaisha tena Al Ahly kupitia shambulizi la kujibu lililowekwa kambani na Trezeguet kwa mara nyingine.

Yanga ilitengeneza nafasi nzuri zaidi kwenye kipindi cha kwanza lakini Maxi Nzengeli na Allan Okello walikosa kuifungia timu yao.

Yanga sasa inarejea Tanzania huku ikifahamu inapaswa kushinda mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki ijayo dimba la New Amaan Complex visiwani Zanzibar.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
2h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
6h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
9h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
12h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
12h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
12h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
18h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’