Local,Normal News,Simba, Esperance

Simba yakubali kipigo dhidi ya Esperance CAFCL

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 Jan 2026
Simba yakubali kipigo dhidi ya Esperance CAFCL

Simba imepoteza mchezo wa tatu mfululizo ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL) ikikubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Esperance huko Tunisia.

Simba iliuanza mchezo huo kwa kasi mapema tu ilipoteza nafasi kupitia kwa Jonathan Sowah baada ya shuti lake ndani ya 18 kuokolewa na mlinda lango wa Esperance.

Bao pekee la Esprance lilifungwa na Jack Diarra akimzidi mbio mlinzi wa kulia wa Simba Shomari Kapombe na kuujaza mpira kimiani kiurahisi.

Simba ilitawala mchezo zaidi kwenye kipindi cha pili lakini hakukuwa na nafasi zilizotengenezwa safu ya ulinzi ya Esperance ikiondoa hatari zote langoni.

Sio matokeo mazuri kwa Simba kwani sasa italazimika kushinda mechi tatu zilizobaki mbili zikiwa nyumbani na moja ugenini.

Mchezo unaofuata ni dhidi ya Esperance ukitarajiwa kupigwa wiki ijayo dimba la Benjamin Mkapa.

Baada ya mchezo huo Simbaa itasalia na mechi mbili dhidi ya Petro Atletico (ugenini) na Stade Malien (nyumbani).

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
3h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
6h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
10h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
12h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
13h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
13h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
15h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
18h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’