Local,Normal News,Yanga, Ismaily

Miloud Hamdi ajiuzulu Ismaily

Joel JJ By Joel JJ
27 Jan 2026
Miloud Hamdi ajiuzulu Ismaily

Aliyekuwa kocha wa Young Africans SC (Yanga) msimu uliopita, Miloud Hamdi, ametangaza kujiuzulu rasmi wadhifa wake wa ukocha katika klabu ya Ismaily SC ya Misri.

Hamdi ametangaza uamuzi huo jana, Jumatatu Januari 26, 2026, baada ya kuitumikia Ismaily kwa kipindi cha miezi sita pekee, tangu alipojiunga na klabu hiyo Julai 3, 2025, akitokea Yanga.

Katika ujumbe wake wa kuaga, Hamdi ameonyesha shukrani kwa uongozi, wachezaji na wafanyakazi wa klabu hiyo, akisisitiza mshikamano waliokuwa nao licha ya changamoto.

Aliyekuwa kocha wa Young Africans SC (Yanga) msimu uliopita, Miloud Hamdi, ametangaza kujiuzulu rasmi wadhifa wake wa ukocha katika klabu ya Ismaily SC ya Misri.

Hamdi ametangaza uamuzi huo jana, Jumatatu Januari 26, 2026, baada ya kuitumikia Ismaily kwa kipindi cha miezi sita pekee, tangu alipojiunga na klabu hiyo tarehe Julai 3, 2025, akitokea Yanga.

Katika ujumbe wake wa kuaga, Hamdi ameonyesha shukrani kwa uongozi, wachezaji na wafanyakazi wa klabu hiyo, akisisitiza mshikamano waliokuwa nao licha ya changamoto.

"Nawashukuru kwa nyakati tulizopita pamoja katika vipindi vigumu. Lakini tulifanikiwa kuwa tumeungana pamoja. Tulikuwa familia halisi na wataalam wa tiba na sekretarieti ya klabu ikiongozwa na Ahmed Salah,” amesema Hamdi.

“Kufuatia kujiuzulu kwangu klabuni, kipekee nitakumbuka nyakati nzuri pamoja na mashabiki wetu. Nawatakia kila la kheri.”

Ingawa kocha huyo hakutaja wazi sababu za kujiuzulu, wachambuzi wa soka wanaeleza kuwa matokeo yasiyoridhisha ya Ismaily chini ya uongozi wake yanaweza kuwa chanzo kikuu cha uamuzi huo.

Tangu Hamdi aanze kazi rasmi Julai mwaka jana, Ismaily imecheza jumla ya mechi 19 katika mashindano mbalimbali, ikifanikiwa kupata ushindi mara nne tu, sare mbili, huku ikipoteza mechi 13—rekodi iliyoiweka klabu hiyo katika presha kubwa kutoka kwa mashabiki na wadau wa soka nchini Misri.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
4h ago
READ MORE →
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
8h ago
READ MORE →
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
10h ago
READ MORE →
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
12h ago
READ MORE →
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
14h ago
READ MORE →
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
14h ago
READ MORE →
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
14h ago
READ MORE →
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
16h ago
READ MORE →
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
20h ago
READ MORE →
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE →