Kiungo mshambuliaji wa zamani wa timu za Singida Black Stars, Mbeya City , KMC na KenGold James Msuva amejiunga na timu ya Coastal Union kama mchezaji huru.
Mchezaji huyo mara ya mwisho alikuwa anaitumikia timu ya KenGold ya Mbeya ambayo ilishuka daraja msimu uliopita.
Tayari Coastal Union imetambulisha usajili wa nyota huyo ambaye ni mdogo wa mshambuliaji wa Taifa Stars, Simon Msuva.

