Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limeufungia uwanja wa kMC Dar es salaam kutumika kwa michezo ya ligi baada ya kukosa vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.
Taarifa iliyotolewa na TFF mapema leo, imebainisha kuwa miundombinu ya uwanja huo haikidhi matakwa ya kikanuni kama inavyoainishwa kwenye masharti ya kanuni ya leseni za klabu.
Kufuatia uamuzi huo, timu zinazotumia dimba la KMC Complex zitalazimika kutumia uwanja mwingine kama kanuni zinavyoelekeza.




