International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Januari 30 2026

Joel JJ By Joel JJ
β€’
30 Jan 2026
Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Januari 30 2026

Wawakilishi wa winga wa England Raheem Sterling, 31, ambaye aliondoka Chelsea kwa makubaliano ya pande zote mapema wiki hii, wako kwenye mazungumzo na vilabu saba vya kiwango cha Ligi ya Mabingwa Ulaya vinavyotaka kumsajili. (Sky Sports)

Tottenham wanaangalia kwa umakini uwezekano wa kumsajili Sterling, ambaye sasa ni mchezaji huru, na kocha Thomas Frank yuko tayari na anaunga mkono uhamisho huo. (Teamtalk) Burnley, pamoja na vilabu vya Italia vya Serie A Juventus na Napoli, pia vina nia ya kumsajili Sterling. (Mail)

Manchester United hawatamsajili kiungo wa Chelsea Cole Palmer, 23, msimu huu wa joto, kwani viongozi wa klabu wanajua kuwa mchezaji huyo wa England yuko nje ya uwezo wao wa kifedha. (Mirror)

Chelsea wanapanga kutumia euro milioni 150 (Β£129m) kumsajili kiungo wa Real Madrid na England Jude Bellingham, 22, msimu huu wa joto. (Fichajes)

Ajax wako tayari kumsajili kiungo wa Ukraine Oleksandr Zinchenko, 29, ambaye yuko kwa mkopo Nottingham Forest kutoka Arsenal, kwa uhamisho wa kudumu wa takriban euro milioni 1.5 (Β£1.3m), pamoja na ziada endapo klabu hiyo ya Uholanzi itafuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya. (Fabrizio Romano)

Kocha wa Aston Villa, Unai Emery, yupo kwenye orodha ya Real Madrid ya makocha wanaoweza kuchukua nafasi ya kuwa kocha mpya msimu huu wa joto. (Sky Germany)

Chelsea bado wako kwenye mazungumzo na Rennes kumsajili beki wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20, Jeremy Jacquet, kabla ya dirisha la usajili la Januari kufungwa. (Givemesport)

Real Madrid wanataka kumsajili beki wa pembeni wa Manchester United na Ureno Diogo Dalot, 26, kutokana na udhaifu wao katika safu ya ulinzi. (Fichajes)

Manchester City wamekubali kumpeleka beki kinda wa England mwenye umri wa miaka 17, Stephen Mfuni, kwa mkopo Watford hadi mwisho wa msimu. (Fabrizio Romano)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
47m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’