Local,Normal News,Azam, Singida

Azam Fc yafufua matumaini CAFCC, Singida BS yapoteza ugenini

Joel JJ By Joel JJ
β€’
2 Feb 2026
Azam Fc yafufua matumaini CAFCC, Singida BS yapoteza ugenini

Ushindi wa bao 1-0 ambao Azam Fc waliupata dhidi ya Nairobi United jana umefufua matumaini ya wauza ice-cream hao katika kuisaka tiketi ya kufuzu robo fainali ya kombe la Shirikisho (CAFCC).

Bao la mapema lililofungwa na Feisal Salum 'Fei Toto' lilidumu kwa dakika zot 90 na kuishuhudia Azam Fc ikiipiga Nairobi United 'nje-ndani' sasa wakifikisha alama 6 kundi B huku Nairobi United wakipoteza matumaini.

Katika mchezo uliopigwa mapema, klabu ya Otoho d’Oyo ya Jamhuri ya Congo ikaibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars ya Tanzania katika mchezo ambao mlinda lango wa Singida BS Metacha Mnata alitolewa nje kwa kadi nyekundu.

Tukio hilo la kadi nyekundu limekuwa mojawapo ya sababu kuu zinazotajwa kuchangia matokeo ya mchezo huo, huku Singida ikilazimika kupambana katika mazingira magumu kwa zaidi ya dakika 60.

Singida BS wako nafasi ya tatu kundi D wakiwa na alama 4 bado wako kwenye mbio za kuisaka robo fainali.

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
4m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
33m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’