Klabu ya Manchester United inajutia uamuzi wake wa kukubali kumuuza mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford kwa Barcelona kwa £26m kwa sababu wanaamini kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 sasa ana thamani ya takriban £50m. (Star)
Beki wa Bournemouth na Argentina Marcos Senesi, 28, anataka kujiunga na kalabu ya Barcelona msimu huu wa joto baada ya kuamua hatasaini mkataba mpya na Cherries. (Team Tal)
Mshambuliaji Muingereza Liam Delap, 23, huenda akaondoka Chelsea msimu huu wa joto, na hivyo kuzua shauku kutoka kwa vilabu vikiwemo Manchester United, Newcastle na Everton. (Caughtoffside)
Manchester United wako tayari kumwachia winga wa Uingereza Jadon Sancho, 25, kuondoka bila malipo mwishoni mwa msimu huu. (Sun) West Ham inaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Canada Promise David mwenye umri wa miaka 24 kutoka Union Saint-Gilloise. (Team Talk)
Tottenham huenda ikatumia fedha nyingi katika usajili wa msimu huu wa joto huku tetesi zikiibuka kwamba inanyatia kiungo wa Aston Villa Muingereza Morgan Rogers mwenye umri wa miaka 23. (Football Insider)
Mshambuliaji wa Tottenham Richarlison anaweza kukihama klabu hicho, huku Flamengo na Atletico Madrid zikionyesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 28. (Fichajes - kwa Kihispania)
BBC