Local,Normal News,Yanga, Simba

Bodi ya ligi yafunguka Kariakoo Dabi kupelekwa Zanzibar

Joel JJ By Joel JJ
β€’
20 Feb 2026
Bodi ya ligi yafunguka Kariakoo Dabi kupelekwa Zanzibar

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imeeleza sababu za kuhamisha Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga Sc na Simba Sc kutoka Uwanja wa Benjamin Mkapa Stadium hadi New Amaan Complex, Zanzibar

Mchezo huo namba 54 wa Ligi Kuu ya NBC unatarajiwa kuchezwa Machi 1, 2026, visiwani Zanzibar badala ya Dar es Salaam kama ilivyopangwa awali.

Akizungumza kuhusu mabadiliko hayo, Afisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Karim Boimanda, amesema sababu kuu ya kuhamisha mchezo huo ni kutokana na Uwanja wa Benjamin Mkapa kuwa na matumizi mengine siku hiyo.

Kwa mujibu wa Boimanda, Machi 1, 2026 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kutafanyika mashindano makubwa ya Mabara yote ya Qur'an ulimwenguni, tukio litakalohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hussein Mwinyi.

Kumekuwa na taarifa kuwa klabu ya Simba iliandikia barua Bodi ya Ligi kuhoji mabadiliko hayo ya uwanja, wakidai hawakupata taarifa rasmi ndani ya muda wa kikanuni kuhusu uamuzi huo.

Bodi ya Ligi imesisitiza kuwa uamuzi wa kuhamisha dabi hiyo umefanyika kwa kuzingatia ratiba na upatikanaji wa viwanja, huku ikihakikisha mchezo huo utachezwa kwa tarehe iliyopangwa lakini katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Dabi ya Kariakoo ni mechi kubwa yenye mvuto zaidi katika Ligi Kuu Tanzania Bara, na uamuzi wa kuipeleka Zanzibar unatarajiwa kuongeza hamasa kwa mashabiki wa soka visiwani humo.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
46m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’