Local,Normal News,Simba

Kocha Simba alia na matumizi ya nafasi

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 Feb 2026
Kocha Simba alia na matumizi ya nafasi

Kocha Mkuu wa Simba Steve Barker ameweka wazi mkakati wake wa kuboresha eneo la umalizia kwa kikosi chake ili kuhakikisha wanatumia vyema nafasi na kufunga mabao mengi.

Barker amesema wanahitaji kuongeza ufanisi mbele ya lango kwani wanatengeneza nafasi nyingi lakini matumizi ya nafasi hizo sio kwa kiwango kikubwa.

Kocha huyo raia wa Afrika Kusini amesema katika ligi yenye ushindani kama hii ya Tanzania Bara, wakati mwingine uwiano wa mabao unaweza kuamua bingwa.

"Nimefurahishwa na ushindi dhidi ya Prisons lakini ukweli ni kwamba tunatengeneza nafasi nyingi na hatuzitumii ipasavyo. Lazima tuwe na makali zaidi mbele ya lango, napenda kumaliza mechi mapema."

"Timu inaendelea kuimarika na ninaamini tutaendelea kufanya vizuri zaidi ya sasa, nina furaha kuona vijana wakipambana kila mmoja katika nafasi yake, akionyesha vile anaweza kuwa msaada kwa timu."

"Wakati mwingine ubingwa unaamuliwa kwa tofauti ya mabao, hivyo hatupaswi kuridhika na ushindi wa bao moja au mawili kama kunakuwa na nafasi za kufunga zaidi,” alisema Barker

Tangu achukue majukumu ya kuinoa Simba, kikosi chake kimefunga mabao matatu katika mechi moja tu ya kombe la CRDB dhidi ya Greenland huku wakicheza mechi saba mfululizo bila ya kupoteza

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
59m ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
10h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
23h ago
READ MORE β†’