Local,Normal News,Simba

Sowah matatani Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 Feb 2026
Sowah matatani Simba

Mshambuliaji wa Simba, Jonathan Sowah, hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoshuka dimbani Jumatano kuikabili Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC, licha ya kumaliza adhabu ya kukosa mechi tano.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa uamuzi wa kumwondoa kwenye mpango wa mchezo huo umefanywa na kocha mkuu, Steve Barker, kufuatia matukio ya kujirudia ya utovu wa nidhamu.

Imeelezwa kuwa mshambuliaji huyo tayari amerejea jijini Dar es Salaam, huku suala lake likitarajiwa kuwasilishwa katika Kamati ya Nidhamu ya klabu kwa hatua zaidi. Endapo atapatikana na hatia, huenda akachukuliwa hatua kali zaidi, ikiwemo kusimamishwa.

Tangu alipoanza kuinoa Simba, Barker amekuwa akisisitiza umuhimu wa nidhamu, akieleza wazi kuwa kila mchezaji anapaswa kuzingatia maadili na taratibu za timu bila kujali hadhi yake kikosini.

Hii ni mara ya pili kwa Sowah kuingia matatani akikabiliwa na tuhuma hizo hizo za utovu wa nidhamu.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
7h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
10h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
12h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
14h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
16h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
17h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
17h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
19h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
22h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’