Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mechi tatu za viporo zinatarajiwa kupigwa katika viwanja mbalimbali.
Mabingwa watetezi Yanga wao watashuka uwanja wa KMC Complex kuwakabili vinara wa ligi hiyo JKT Tanzania katika mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali.
Nao Wekundu wa Msimbazi, Simba Sc watakuwa mkoani Dodoma kuikabili Dodoma Jiji katika mechi nyingine inayotarajiwa kuwa na msisimko.
Mchezo utakohitimisha ratiba ya leo ni kati ya Azam Fc dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa uwanja wa Azam Complex.




