Local,Normal News,Yanga, JKT

Yanga yaifumua JKT Tanzania 5-0, yapanda kileleni

Joel JJ By Joel JJ
β€’
25 Feb 2026
Yanga yaifumua JKT Tanzania 5-0, yapanda kileleni

Yanga imetuma salamu kwa watani zao Simba ambao wanakutana nao katika mchezo unaofuata wakiichapa JKT Tanzania mabao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa KMC Complex.

Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' ndiye aliyefunga bao la mapema kipindi cha kwanza akimalizia pasi ya Prince Dube ambaye awali kulikuwa na taarifa angekosa mchezo wa leo lakini amerejea kwa wakati.

JKT Tanzania walihimili mikiki mikiki ya Yanga kwenye kipindi cha kwanza kwani mpaka mapumziko walikuwa wamefungwa bao moja tu.

Hata hivyo vijana wa kocha Pedro Goncalves walirejea kipindi cha pili wakiwa moto zaidi wakifanikiwa kuongeza mabao manne.

Laurindo Aurelio 'Depu' ameendeleza kasi yake ya kuweka mipira kimiani akifunga bao la pili baada ya krosi ya Israel Mwenda huku Mudathir Yahya akiongeza bao la tatu dakika mbili baadae akimalizia mpira uliogongwa mwamba.

Dube ambaye alichaguliwa nyota wa mchezo akaweka kambani bao la nne akimalizia krosi ya Buba Jammeh huku Shakhan Khamis akipigilia msumari wa tano dakika za lala salama.

Wachezaji wa Yanga leo ni kama walisikia maoni ya mashabiki wao baada ya kutocheza vyema mchezo uliopita. Walikuwa hatari kila waliposhambulia lango la JKT Tanzania.

Ni ushindi ambao umeirudisha rasmi Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi wakiishusha JKT Tanzania hadi nafasi ya piili.

More Stories

Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
3h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
5h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
7h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
9h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
9h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
10h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
12h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
15h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
22h ago
READ MORE β†’
Wapinzani wa Simba, Mighty Wanderers kutua nchini leo wakitokea Malawi
Wapinzani wa Simba, Mighty Wanderers kutua nchini leo wakitokea Malawi
1d ago
READ MORE β†’