Local,Normal News,Yanga, Simba

Kariakoo Derby; Yanga yatangulia Zanzibar

Joel JJ By Joel JJ
β€’
26 Feb 2026
Kariakoo Derby; Yanga yatangulia Zanzibar

Homa ya pambano la watani wa jadi ligi kuu ya NBC kati ya Yanga dhidi ya Simba inazidi kupanda zikisalia takribani siku nne tu mchezo huo kupigwa visiwani Zanzibar.

Mchezo huo namba 54 utapigwa uwanja wa New Amaan Complex siku ya Jumapili, March 1 saa 3 usiku.

Klabu ya Yanga imeondoka mapema leo jijini Dar es salaam kuelekea Zanzibar kukamilisha maandalizi yake huku watani zao Simba wakitarajiwa kurejea jijini Dar es salaam leo wakitokea Dodoma ambako jana walilazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.

Kocha Mkuu wa Simba Steve Barker amesema kikosi chake kitaelekea Zanzibar mapema ili kupata muda wa kukamilisha maandalizi kuelekea mtanange huo.

Simba inaweza kuwa kwenye presha kubwa ya matokeo pengine kuliko Yanga kufuatia matokeo ya sare waliyopata jana.

Yanga iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 28 baada ya mechi 10 huku Simba ikishika nafasi ya tatu ikiwa na alama 23 baada ya mechi 10.

Tayari Yanga inaizidi Simba alama 5 hivyo kama watapoteza mchezo huo Jumapili watakuwa nyuma ya Yanga kwa alama nane ambapo watajiweka katika mazingira magumu kwenye mbio za ubingwa.

Lakini pia Yanga imeshinda mechi nne mfululizo zilizopita kwenye ligi, Wananchi watakuwa wakisaka rekodi nyngine ya kuendeleza ubabe dhidi ya watani zao hao

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’