International,Normal News,

Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa February 27 2026

Joel JJ By Joel JJ
β€’
27 Feb 2026
Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa February 27 2026

Liverpool imo katika mpango thabiti wa kumnunua beki wa Nottingham Forest na Brazil Murillo, 23, ingawa Chelsea bado wanaongoza mbio za kumnunua mchezaji huyo. (TeamTalks)

Ripoti kwamba Jurgen Klopp ataacha jukumu lake kama mkuu wa soka duniani katika shirika la Red Bull "ni upuuzi mtupu na hazina msingi kabisa," anasema Mkurugenzi Mtendaji Oliver Mintzlaff. (Sky Sports Ujerumani - kIn Germany)

Mchezaji wa kimataifa wa Serbia Dusan Vlahovic anapendelea kuhamia Barcelona wakati kandarasi yake ya Juventus itakapokamilika msimu huu wa joto, ingawa Tottenham Hotspur na Chelsea bado wanawinda saini ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (TeamTalks)

Arsenal na Manchester City wanafikiria kuweka dau la Β£30m kumnunua beki wa kushoto wa Atalanta Honest Ahanor. Chelsea pia wanavutiwa na Mnigeria huyo mwenye umri wa miaka 18. (Caught Offside)

Liverpool na Manchester United hawatalipa bei ya Wolves ya pauni milioni 50 kwa ajili ya mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Mateus Mane mwenye umri wa miaka 18 msimu huu kwa sababu wanamchukulia kiungo huyo kuwa mbichi sana. (Football Insider)

Mshambulizi wa zamani wa Brentford Ivan Toney analenga kushinda mataji nchini Saudi Arabia na klabu ya sasa ya Al-Ahli, lakini Muingereza huyo, 29, hataki kurejea kwenye Ligi ya Premia. (Sportsport)

Mshambulizi Nicolas Jackson anatarajiwa kurejea Chelsea. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal mwenye umri wa miaka 24 alihamia Bayern Munich kwa mkopo msimu uliopita wa joto, lakini mabingwa hao wa Bundesliga hawataki uhamisho wa kudumu. (CFBayernInsider).

Newcastle United inamchunguza mlinda lango wa Brighton na Uholanzi Bart Verbruggen na mlinda lango wa Manchester City James Trafford, wote 23, wakilenga kutafuta mrithi wa muda mrefu wa mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Nick Pope, 33. (The i Newspaper - Subscription Required)

Newcastle United pia inamwangalia winga wa Union Saint-Gilloise Anan Khalaili. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Israel mwenye umri wa miaka 21 amefunga mara tatu kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu. (Mail+ - Subscription Required)

Winga wa Liverpool Trent Kone-Doherty, 19, kutoka Ireland Kaskazini, huenda akaondoka hivi karibuni na kujiunga na klabu ya Molde ya Norway licha ya kupewa kandarasi mpya huko Anfield. (Football Insider)

Napoli iliweka kipengele katika mkataba wa uhamisho wa mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen kwenda Galatasaray ambayo ina maana kwamba klabu hiyo ya Uturuki italazimika kuwalipa hadi Β£60m ikiwa watamuuza mchezaji huyo wa miaka 27 kwa klabu ya Italia. (Gazzetta dello Sport - In Italy)

BBC

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
58m ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
10h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
23h ago
READ MORE β†’