Local,Normal News,Yanga, Simba

Waamuzi wa dabi ya Kariakoo watahadharishwa mapemaa

Joel JJ By Joel JJ
28 Feb 2026
Waamuzi wa dabi ya Kariakoo watahadharishwa mapemaa

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema mwamuzi yoyote atakayeharibu mchezo wa kesho wa dabi ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba, watamfungia maisha kujihusisha na mpira wa miguu.

Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa TFF unaofanyika Kahama mkoani Shinyanga mapema leo, Karia alisema mbali na kumfungia maisha pia watamfungulia mashataka.

“Naomba niseme hapa kwenye Mkutano Mkuu na waamuzi wanisikie, atakayeharibu mchezo wa kesho hatutamuacha salama, malalamiko yamekuwa mengi na yanaharibu taswira ya mchezo,” alisema Karia.

Jana Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilimtangaza Nassor Mwinchui mwamuzi kutoka Tanga ndiye mwamuzi wa kati mchezo kati ya Yanga dhidi ya Simba utakaopigwa kesho Jumapili, March 1 katika uwanja wa New Amaan Complex.

Mwamuzi Msaidizi I ni Kassim Mpanga kutoka Dar es salaam wakati Msaidizi II ni Hamdan Said kutoka Mtwara,

Ramadhan Kayoko ni mwamuzi wa akiba na Israel Mjui akiwa mtathmini waamuzi.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE →
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE →
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE →
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE →
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE →
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE →
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE →
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE →
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE →
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
23h ago
READ MORE →