Local,Normal News,Yanga, Simba

Yanga na Simba hakuna mbabe New Amaan Complex

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1 Mar 2026
Yanga na Simba hakuna mbabe New Amaan Complex

Mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya Yanga dhidi ya Simba uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex, umemalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana.

Unaweza kusema timu bora leo Simba imenyimwa alama tatu kwani Suleiman Mwalimu alifunga bao halali ambalo lilikataliwa kimakosa na mwamuzi msaidizi Kasim Mpanga.

Simba iliuanza mchezo huo kwa kasi na pengine Inno Loemba na Annicet Oura wangeweza kufunga bao mapema kama sio uimara wa golikipa wa Yanga Djigui Diarra.

Dakika zote 45 za kipindi cha kwanza ni Simba iliyokuwa bora uwanjani kilichokosekana ni mabao tu.

Kipindi cha pili mwanzoni Yanga ilikuwa bora lakini kuanzia dakika ya 60 ni Simba iliyorejesha umiliki wa mechi na Mwalimu aliyeingia kipindi cha pili alifunga bao lililokataliwa kwa offside.

Elie Mpanzu nae aliyeingia dakika ya 75 kipindi cha pili alikosa nafasi wakati mchezo huo ukielekea ukingoni.

Ni kiwango bora kwa Simba katika mchezo huo, pengine hii ni dalili njema kwa Simba kwenye mbio za ubingwa.

Matokeo hayo yanaendelea kuiweka Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi ikifikisha alama 29 huku Simba ikiendelea kusalia nafasi ya tatu ikiwa na alama 24.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
5h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
8h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
10h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
12h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
14h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
15h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
15h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
20h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’