Chelsea wameibuka kuwa wapinzani watarajiwa wa Newcastle United katika kuwania saini ya mchezaji wa kimataifa wa Uruguay Darwin Nunez. Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 26 amesalia katika orodha ya wachezaji wa akiba katika klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia inayompendelea mshambuliaji wa Ufaransa Karim Benzema mwenye umri wa miaka 38. (Chronicle Live)





