International,Normal News,

Iran kukacha kombe la Dunia Marekani?

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Mar 2026
Iran kukacha kombe la Dunia Marekani?

Rais wa Shirikisho la Soka la Iran, Mehdi Taj, amesema hajui kama Timu yao ya Taifa itaweza kushiriki fainali za Kombe la Dunia baada ya mashambulizi ya Marekani na Israeli dhidi ya nchi yake.

"Kilicho hakika ni baada ya mashambulio haya, hatuwezi kutarajiwa kushiriki Kombe la Dunia," amesema Taj akiiambia tovuti ya michezo Varzesh3 huku Iran ikishambuliana na Israeli kama sehemu ya vita vinavyoendelea.

Mashambulizi ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran yanaendelea baada ya kuuawa kwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, na hilo linaifanya nchi hiyo kutokuwa na uhakika na kuongeza hatari ya kutokuwa na utulivu wa ukanda huo wa Mashariki ya Kati.

Iran imepangwa katika Kundi G kwenye Kombe la Dunia na mechi zake itacheza jijini Los Angeles ambapo itakabiliana na New Zealand na Ubelgiji mnamo Juni 15 na Juni 21, kabla ya kucheza na Misri huko Seattle Juni 26, mwaka huu.

Marekani itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo pamoja na Canada na Mexico kuanzia Juni 11 hadi Julai 19, mwaka huu.

Mashabiki kutoka Iran tayari walikuwa wamezuiwa kuingia Marekani katika awamu ya kwanza ya marufuku ya usafiri iliyotangazwa na utawala wa Rais Donald Trump.

FIFA haikuwa tayari kutoa maelezo yoyote kutoka kwa Shirika la Habari la The Associated Press lililotaka kujua kuhusu hali ya sasa na ushiriki wa Iran katika Kombe la Dunia.

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
3m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
32m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’