Local,Normal News,Azam, Yanga

Azam Fc vs Yanga kupigwa Chamazi

Joel JJ By Joel JJ
3 Mar 2026
Azam Fc vs Yanga kupigwa Chamazi

Mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya Azam Fc dhidi ya Yanga ulipangwa kuchezwa March 15, umehamishiwa uwanja wa Azam Complex baada ya uwanja wa Benjamin Mkapa kufungwa kwa ajili ya ukarabati.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ amethibitisha kuwa mchezo huo wa kwanza dhidi ya Yanga katika ligi utachezwa Uwanja wa Azam Complex.

“Mechi hiyo itachezwa hapa uwanja wa nyumbani na siyo kwa Mkapa kama ilivyozoeleka, hivyo tunawakaribisha sana mashabiki waje kushuhudia mechi kubwa na nzuri,” alisema Zaka Zakazi.

Msimu uliopita mechi zote mbili za Ligi Kuu Bara zilizokutanisha timu hizo zilipigwa uwanjani hapo. Mechi ya duru kwanza Azam Fc iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Gibril Sillah, kisha duru la pili Yanga ikashinda 2-1. Mabao ya Yanga yalifungwa na Pacome Zouzoua na Prince Dube wakati Azam mfungaji alikuwa Lusajo Mwaikenda.

Kwa sasa Azam inashika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 23, wakati Yanga ikiongoza na pointi 29, zote zimecheza mechi 11.

Kabla ya dabi hiyo, zote zitashuka dimbani mara tatu, zikiwamo mechi mbili za ligi na moja Kombe la Shirikisho (FA).

Machi 5, Yanga itacheza dhidi ya Singida Black Stars wakati Azam ikipambana na Tanzania Prisons, katika mechi za Ligi Kuu Bara zote zikiwa ugenini.

Machi 8, zote zitakuwa nyumbani katika hatua ya 32 Bora ya Kombe la Shirikisho (FA), Yanga ikicheza dhidi ya Polisi Tanzania na Azam dhidi ya Mbeya Kwanza.

Machi 11, Azam itakuwa ugenini kucheza dhidi ya Dodoma Jiji, kisha Machi 12, Yanga pia itakuwa ugenini kucheza dhidi ya Tanzania Prisons.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
4h ago
READ MORE →
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
8h ago
READ MORE →
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
9h ago
READ MORE →
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
11h ago
READ MORE →
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
14h ago
READ MORE →
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
14h ago
READ MORE →
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
14h ago
READ MORE →
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
16h ago
READ MORE →
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
20h ago
READ MORE →
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE →