International,Normal News,Local, Chelsea, Manchester City, Arsenal, Newcastle

Arsenal, Man City, Chelsea zapeta kombe la FA

Joel JJ By Joel JJ
8 Mar 2026
Arsenal, Man City, Chelsea zapeta kombe la FA

Michuano ya FA Cup iliendelea Jumamosi usiku, Machi 7, 2026 kwa michezo ya hatua ya raundi ya tano (Fifth Round), ambapo vigogo kadhaa wa soka la England waliibuka na ushindi na kufuzu hatua ya robo fainali.

Timu zilizofanikiwa kusonga mbele ni pamoja na Manchester City, Chelsea na Arsenal, huku baadhi ya timu ndogo zikionyesha ushindani mkali dhidi ya vigogo hao.

Manchester City Waiondoa Newcastle

Katika mchezo mkubwa wa usiku huo, Manchester City waliibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Newcastle United katika dimba la St. James’ Park.

Newcastle walikuwa wa kwanza kupata bao, lakini City walirejea kwa nguvu kipindi cha pili ambapo mshambuliaji Omar Marmoush alifunga mabao mawili na kuihakikishia timu yake ushindi na tiketi ya robo fainali. 

Ushindi huo uliendelea kudumisha matumaini ya City ya kutwaa kombe hilo msimu huu.

Chelsea Waibuka na Ushindi Baada ya Dakika za Nyongeza

Mchezo uliovuta hisia nyingi ulikuwa kati ya Wrexham na Chelsea, ambapo Chelsea walishinda 4-2 baada ya muda wa nyongeza.

Wrexham waliwapa upinzani mkubwa wageni wao na hata kuongoza mara mbili ndani ya dakika 90. Hata hivyo Chelsea walisawazisha na kulazimisha dakika za nyongeza.

Katika muda huo wa ziada, Alejandro Garnacho alifunga bao muhimu kabla ya João Pedro kufunga bao la mwisho na kuhitimisha ushindi huo wa kusisimua.

Arsenal Wapita Kwa Mbinde

Kwa upande mwingine, Arsenal walilazimika kupambana hadi mwisho kabla ya kuifunga Mansfield Town kwa mabao 2-1.

Arsenal walipata bao la kwanza kupitia Noni Madueke, lakini Mansfield walisawazisha mapema kipindi cha pili.

Hata hivyo, kiungo Eberechi Eze alifunga bao muhimu lililoipeleka Arsenal hatua ya robo fainali.

Matokeo hayo yamefanya mbio za ubingwa wa FA Cup msimu wa 2025/26 kuendelea kushika kasi huku timu kubwa zikiendelea kusalia katika mashindano hayo.

Hatua inayofuata ni robo fainali, ambapo vigogo hao watapambana kuwania nafasi ya kufika fainali katika dimba la Wembley Stadium.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE →
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE →
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE →
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE →
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE →
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE →
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE →
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE →
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE →
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
23h ago
READ MORE →