Local,Normal News,Yanga

Beki Yanga afanyiwa upasuaji Afrika Kusini

Joel JJ By Joel JJ
β€’
11 Mar 2026
Beki Yanga afanyiwa upasuaji Afrika Kusini

Klabu ya Yanga imethibitisha kuwa nahodha wake msaidizi Dickson Job amefanyiwa upasuaji wa goti Afrika Kusini.

Job ambaye ni beki tegemeo wa Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', alipata majeraha kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex mapema mwezi huu na kumalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana.

Job alipata majeraha hayo baada ya kugongana na kiungo mshambuliaji wa Simba Inno Loemba na kulazimika kutoka nje nafasi yake ikichukuliwa na Bakari Mwamnyeto.

Job anatarajiwa kuwa nje kwa takribani wiki nane au zaidi kutegemeana na uponaji wa jeraha lake baada ya upasuaji huo uliofanikiwa.

Yanga itamkosa beki huyo katika kipindi muhimu ambacho wanakabiliwa na mechi mfululizo.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
5h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
11h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
17h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’