Local,Normal News,Yanga, Prisons

Yanga yaichapa Prisons 1-0 Dodoma

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Mar 2026
Yanga yaichapa Prisons 1-0 Dodoma

Yanga imeendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi ikiichapa Tanzania Prisons bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Mshambuliaji Laurindo Aurelio ndiye aliyepeleka kilio kwa maafande hao akifunga bao dakika ya 78 akimalizia mpira uliotemwa na mlinda lango Moussa Mbissa baada ya shuti la Allan Okello kupitia mpira w adhabu.

Depu aliingia kipindi cha pili na alihitaji takribani dakika 10 tu kuifungia Yanga bao hilo katika mchezo ambao mpango wa Prisons ulikuwa kulinda lango lao.

Ulikuwa mchezo wa upande mmoja kwa muda mwingi Yanga ikitawala lakini haikuwa rahisi kulipenya lango Prisons kabla ya bao la Depu.

Ni alama tatu zinazoifanya Yanga ifikishe alama 35 na hivyo kuendelea kujiweka juu ya msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 7.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
5h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
11h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
17h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’