Local,Normal News,Simba, TRA

Barker aweka hadharani mikakati ya kuikabili TRA United

Joel JJ By Joel JJ
β€’
13 Mar 2026
Barker aweka hadharani mikakati ya kuikabili TRA United

Kocha Mkuu wa Simba Steve Barker amesema amekiandaa kikosi chake kikamilifu kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya TRA United utakaopigwa kesho Jumamosi, March 14 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Barker amesema ligi ni ngumu na wanapaswa kucheza katika kiwango bora kwenye kila mchezo.

Kocha huyo wa zamani wa Stellenbosch ya Afrika Kusini, amesema nyota wake wote wako tayari kwa mchezo huo na dhamira yao ni kuondoka na alama zote tatu kama walivyofanya kwenye mchezo uliopita dhidi ya Singida BS.

"Sisi tumejiandaa vyema kwa ajili ya mchezo, nafahamu hautakuwa mchezo mwepesi. Kila mechi ni ngumu na tunapaswa kucheza katika ubora wetu kupata mtokeo mazuri."

"Ni lazima tucheze kwa kuzingatia mpango tulioandaa kwa ajili ya mchezo huu, nafahamu kama hatutafanya hivyo mchezo unaweza kuwa mgumu."

"Tumekuwa na maandalizi ya kimbinu kwa zaidi ya miezi miwili sasa, maandalizi yetu hayazingatii mchezo mmoja bali tunajiandaa kimfumo na kuhakikisha tunatimiza mipango yetu katika kila mechi. Tunataka kumiliki mchezo na kuwapa wapinzani wetu wakati mgumu katika muda wote wa mchezo," alisema Barker.

Simba ilitua Arusha jana ambao leo inatarajiwa kukamilisha maandalizi yake ya mwisho katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo mchezo huo utapigwa.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’