International,Normal News,Local, Real Madrid, Chelsea, Manchester City, Arsenal, PSG

Real Madrid, Arsenal zapeta robo fainali, Man City, Chelsea zatupwa nje UEFA CL

Joel JJ By Joel JJ
18 Mar 2026
Real Madrid, Arsenal zapeta robo fainali, Man City, Chelsea zatupwa nje UEFA CL

Michuano ya UEFA Champions League imeendelea kushika kasi barani Ulaya huku baadhi ya timu vigogo zikitinga hatua ya robo fainali baada ya mechi za mkondo wa pili wa hatua ya 16 bora zilizochezwa Jumanne, Machi 17, 2026.

Miongoni mwa matokeo makubwa ya usiku huo, Paris Saint-Germain iliibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Chelsea FC, na kufuzu kwa jumla ya mabao 8-2. PSG walionyesha ubora mkubwa katika mchezo huo, wakitawala sehemu kubwa ya dakika 90.

Katika mechi nyingine iliyovuta hisia za mashabiki wengi, Real Madrid iliichapa Manchester City kwa mabao 2-1 ugenini, ushindi uliowapa tiketi ya robo fainali kwa jumla ya mabao 5-1. Nyota wa Madrid, Vinícius Júnior, alikuwa mhimili kwa kufunga mabao yote mawili.

Nayo Arsenal FC iliendeleza kiwango bora baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Bayer Leverkusen, matokeo yaliyowawezesha kusonga mbele katika hatua inayofuata ya mashindano.

Kwa upande mwingine, mechi kati ya Sporting CP na Bodø/Glimt ilikuwa sehemu ya ratiba ya siku hiyo huku timu ya Bodø/Glimt wakiondoshwa michuanoni kwa kipigo cha mabao 5-0, Sporting wametinga robo fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-3

Ratiba ya Mechi za Leo

Michuano hiyo inaendelea leo Jumatano, Machi 18, 2026, kwa michezo mingine ya mkondo wa pili wa hatua ya 16 bora, ambapo vigogo kadhaa wanatarajiwa kushuka dimbani kuwania nafasi za robo fainali.

Miongoni mwa mechi zinazotarajiwa ni ile kati ya FC Barcelona dhidi ya Newcastle United, mchezo unaotarajiwa kuwa mkali kufuatia sare ya 1-1 katika mechi ya kwanza.

Aidha, Bayern Munich watakuwa na kibarua chepesi wanapokutana na Atalanta BC, baada ya ushindi mkubwa wa mabao 6-1 walioupata katika mchezo wa awali.

Katika michezo mingine, Liverpool FC watakuwa na kazi ngumu ya kusaka ushindi dhidi ya Galatasaray SK, huku Tottenham Hotspur wakikabiliana na Atlético Madrid katika pambano lingine lenye ushindani mkali.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE →
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE →
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE →
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE →
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE →
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE →
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE →
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE →
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE →
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE →