Local,Normal News,Yanga, TRA

TRA United, Yanga wagawana pointi

Joel JJ By Joel JJ
β€’
18 Mar 2026
TRA United, Yanga wagawana pointi

Mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya TRA United dhidi ya Yanga uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha umemalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana.

Ni mchezo ambao haukuwa na mashambulizi mengi, wenyeji TRA United wakikaa nyuma kuzuia wakitumia mashambulizi ya kushitukiza huku Yanga licha ya kutawala mchezo kwa muda mwingi, walikosa kasi katika kutengeneza mashambulizi yao.

TRA United walimaliza wakiwa 10 baada ya Mzamiru Yassin kutolewa nje dakika ya 75 akionyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya kumfanyia madhambi Mohamed Hussein.

Dakika za lala salama TRA United walifanya shambulizi kubwa ambalo Yanga watamshukuru mlinda lango Djigui Diarra aliyewaweka salama na kuondoka na alama moja

Ni sare ya pili mfululizo Yanga wanapata huku ikiwa ni sare ya nne msimu huu. Bado Yanga inaendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi ikifikisha alama 37.

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
1h ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
11h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
11h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
12h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
15h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
18h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
19h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
20h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
20h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
21h ago
READ MORE β†’