Klabu ya Singida Black Stars imeendelea kuonyesha makali yake katika Ligi Kuu ya NBC baada ya kuibuka na ushindi muhimu wa mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo uliochezwa Machi 18, 2026.
Katika pambano hilo lililokuwa na ushindani mkubwa, Tanzania Prisons walikuwa wa kwanza kupata bao mapema kupitia mkwaju wa penalti uliofungwa na George Mpole dakika ya 4.





