Local,Normal News,Simba, Pamba, Mashujaa, Azam

Simba, Pamba Jiji, Azam Fc, Mashujaa viwanjani leo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Mar 2026
Simba, Pamba Jiji, Azam Fc, Mashujaa viwanjani leo

Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mechi mbili zinatarajiwa kupigwa mkoani Mwanza na kule Kigoma mwisho wa reli.

Jijini Mwanza Simba Sc itakuwa ugenini kuikabili Pamba Jiji kwenye mchezo utakaopigwa saa 10 jioni.

Ni wazi utakuwa mchezo mgumu unaozikutanisha timu mbili ambazo kwenye mechi zilizopita kati yao, nyasi ziliumia.

Pamba Jiji imeufanya uwanja wa CCM Kirumba kuwa mgumu kwa wapinzani msimu huu, wakulima hao wa Pamba wakishika nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi.

Hata hivyo wanakutana na Simba ambayo kwa sasa imeimarika zaidi ikionyesha dhamira ya kurejesha taji la ligi kuu Msimbazi baada ya kulikosa kwa misimu minne iliyopita.

Simba ilitua jijini Mwanza juzi usiku, jana vijana wa kocha Steve Barker wakafanya mazoezi yao ya mwisho katika dimba la CCM Kirumba.

Baada ya watani zao Yanga kudondosha alama katika mechi mbili zilizopita, hii ni nafasi kwa Simba kupunguza gap la pointi baina ya timu hizo.

Kimahesabu kama Simba itashinda mechi zake zote za viporo, gap la pointi kati yake ya Yanga itasalia alama moja tu hatua ambayo itaweka wazi zaidi mbio za ubingwa wa ligi msimu huu.

Mchezo mwingine utapigwa Kigoma ambapo Mashujaa Fc wataialika Azam Fc kutoka jijini Dar es salam.

Hii ni mechi nyingine ngumu inayotarajiwa kuwa na upinzani mkali. Tangu ujio wa kocha Jamhuri Kiwhelo 'Julio' kwenye kikosi cha Mashujaa Fc, kuna upepo umebadilika.

Azam Fc watahitaji kufanya kazi ya ziada kuondoka na alama zote tatu mbele ya Mashujaa.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
47m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’