Local,Normal News,Yanga

Mwenendo usioridhisha wamuweka matatani kocha Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
23 Mar 2026
Mwenendo usioridhisha wamuweka matatani kocha Yanga

Wakati tetesi zikiendelea kushika kasi juu ya hatma ya kocha mkuu wa Yanga Pedro Goncalves, ni wazi wananchi wanahitaji kutumia vyema kipindi hiki cha mapumziko ya FIFA kujiimarisha ili warejee wakiwa imara zaidi.

Licha ya kuendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi, mwenendo wa mabingwa hao watetezi katika mechi za karibuni umewapa mashaka mashabiki ambao wanaamini kama hakutakuwa na mabadiliko huenda msimu huu wakawa na kazi ngumu ya kutetea ubingwa wao.

Ukiacha changamoto ya mejeruhi na ratiba ngumu, malalamiko yalianza mapema tangu wakati Yanga inashiriki michuano ya ligi ya mabingwa, ikikomea hatua ya makundi baada ya kumaliza nafasi ya tatu kundi B.

Mpaka sasa baada ya kucheza mechi 16 za ligi, Yanga iko nyuma ya kile walichofanya msimu uliopita. Wamekusanya alama 38 alama 4 pungufu ya zile walizokusanya msimu uliopita katika nyakati kama hizi

Msimu uliopita Yanga ilitwaa taji la ligi kuu na pointi 82 baada ya kucheza jumla ya mechi 30, ikishinda 27, sare moja na kupoteza mbili, huku ikifunga mabao 83 yakiwa mengi zaidi kuliko timu nyingine na kuruhusu kumi, ambayo ni machache zaidi.

Hata hivyo mpaka sasa Yanga imedondosha alama 10 katika mechi 16, wakati msimu uliopita walidondosha alama nane tu katika mechi 30.

Yanga imetoka sare tano dhidi ya Mbeya City, Simba, TRA Unted, Azam na Mtibwa Sugar na hivyo kudondosha idadi hiyo ya pointi wakati msimu uliopita timu hiyo ilitoka sare mchezo mmoja pekee dhidi ya JKT Tanzania na ikapoteza michezo miwili dhidi ya Azam na Tabora United (TRA).

Mabosi wa Yanga wanatarajiwa kukutana kujadili mwenendo huo wa timu na haitashangaza yakifanyika mabadiliko kwenye benchi la ufundi.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
5h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
8h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
10h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
12h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
14h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
15h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
15h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
20h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’