Salamba aikacha Coastal Union kisa deni

Joel JJ By Joel JJ β€’ 27th March 2026


Salamba aikacha Coastal Union kisa deni

Mshambuliaji wa Coastal Union, Adam Salamba, inaelezwa kuwa amejiweka kando na kikosi cha timu hiyo hadi pale atakapolipwa malimbikizo ya fedha zake za usajili

Salamba, aliyejiunga na Coastal Union Agosti 1, 2025, ameshaondoka kambini na hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachochuana na Simba Aprili 2, 2026, hadi hapo stahiki zake zitakapolipwa, kwa mujibu wa Mwanaspoti.

Uongozi wa Coastal Union umekiri kuwepo kwa deni hilo na kusema mchakato wa kumlipa unaendelea, huku wakitamani mchezaji huyo angeendelea na mazoezi wakati taratibu zikikamilishwa.

Salamba amewahi kuzitumikia klabu kadhaa ikiwemo Simba, Namungo, na Stand United, pamoja na kucheza soka la kulipwa nchini Libya, Misri, na Kuwait.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.