Kikosi cha Azam Fc kimeondoka jijini Dar es salaam mapema leo kuelekea mkoani Singida tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Black Stars.
Mchezo huo utapigwa siku ya Jumatano, April 1 katika uwanja wa Airtel huko Singida.
Wauza Ice Cream hao wameondoka Dar mapema Jumapili kwa kutumia usafiri wa traini SGR hadi mkoani Dodoma ambako wanatarajiwa kuweka kambi ya muda mfupi kabla ya kuelekea Singida.
Azam Fc wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 29 ambapo ushindi unaweza kuwasogeza hadi nafasi ya pili wakati wenyeji wao Singida BS wanashinda nafasi ya 6 wakiwa na alama 25.


