International,Normal News,Italy, FIFA, Inter, Juventus, Napoli, Milan

Viongozi wakuu wa soka Italia wajiuzulu kufuatia kushindwa kufuzu kombe la Dunia

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Apr 2026
Viongozi wakuu wa soka Italia wajiuzulu kufuatia kushindwa kufuzu kombe la Dunia

Soka la Italia limeingia katika kipindi kigumu baada ya viongozi wakuu wa timu ya taifa kujiuzulu kufuatia kushindwa kufuzu kwa Kombe la Dunia, tukio lililozua mjadala mkubwa nchini humo na kimataifa.

Rais wa Shirikisho la Soka Italia (FIGC), Gabriele Gravina, ametangaza rasmi kuachia ngazi akichukua dhamana ya matokeo mabaya ya timu ya taifa. Hatua hiyo imekuja kufuatia presha kubwa kutoka kwa wadau wa michezo na viongozi wa kisiasa waliotaka mageuzi ya haraka ndani ya soka la nchi hiyo.

Sambamba na uamuzi huo, Mkuu wa Msafara wa timu ya taifa, Gianluigi Buffon, naye ametangaza kujiuzulu, akieleza kuwa ni hatua ya kuwajibika kwa kushindwa kwa timu hiyo kufikia malengo yake ya kufuzu.

Katika upande wa benchi la ufundi, kocha mkuu Gennaro Gattuso nae ameachia wadhifa wake kufuatia matokeo hayo mabaya.

Italia, mabingwa wa dunia mara nne, imeendelea kukumbwa na anguko la kiwango katika miaka ya karibuni, na kushindwa kufuzu kwa Kombe la Dunia mara ya pili mfululizo kumezidisha hali hiyo. Kushindwa huko kumeibua hasira kutoka kwa mashabiki na wachambuzi wa soka, waliotaka mabadiliko ya kina katika mfumo wa maendeleo ya soka nchini humo.

Shirikisho la soka la Italia linatarajiwa kuitisha mkutano maalum wa dharura kujadili mustakabali wa timu ya taifa, ikiwa ni pamoja na uteuzi wa uongozi mpya na maboresho ya kiufundi yatakayolenga kurejesha hadhi ya Italia katika soka la kimataifa.

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
4m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
33m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’