Local,Normal News,Yanga, Prisons, Mashujaa, JKT, Pamba, Namungo

NBC PL : Yanga na Prisons kitaeleweka KMC Complex, mechi tatu kupigwa leo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
4 Apr 2026
NBC PL : Yanga na Prisons kitaeleweka KMC Complex, mechi tatu kupigwa leo

Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo amapo mechi tatu zinatarajiwa kupigwa katika viwanja mbalimbali.

Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga watakuwa dimba la nyumbani KMC Complex kuikabili Tanzania Prisons katika mchezo ambao utapigwa saa 12:30 jioni.

Baada ya kukosa ushindi katika mechi tatu zilizopita, ni wazi Wananchi leo 'wataikamia' Tanzania Prisons ambayo hata hivyo licha ya kuyumba msimu huu, kwenye mechi zilizopita wameonyesha wanaweza kupambana.

Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikiwa imepata 'ahueni' baadhi ya nyota wake waliokuwa majeruhi wakirejea baada ya kupona.

Washambuliaji Prince Dube na Laurindo Aurelio 'Depu' wote walishiriki mazoezi ya mwisho ya Wananchi kuelekea mchezo huo na pengine huenda wakarejea kikosini leo sambamba na walinzi Ibrahim Hamad na Chadrack Boka.

Mechi ya mapema saa 10 itakuwa kule Kigoma dimba la Lake Tanganyika wakati wenyeji Mashujaa Fc watakapomenyana na Pamba Jiji katika mchezo mwingine unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali.

Pamba Jiji wamekuwa na msimu bora mpaka sasa wakipania kumaliza nafasi nne za juu kwenye msimamo huku Mashujaa Fc nao wakijipanga upya chini ya kocha Jamhuri Kiwhelo 'Julio' baada ya kuyumba mwanzoni mwa msimu.

Namungo Fc wataikaribisha JKT Tanzania katika mchezo mwingine wa kukata na shoka ambao utapigwa uwanja wa Majaliwa saa 3 usiku.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
37m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’