International,Normal News,Local, Barcelona, Atletico, Real Madrid

Barcelona yaichapa Atletico, ubingwa wanukia Catalunya

Joel JJ By Joel JJ
5 Apr 2026
Barcelona yaichapa Atletico, ubingwa wanukia Catalunya

Klabu ya Barcelona imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa La Liga baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Atletico Madrid katika mchezo mkali uliopigwa jijini Madrid.

Ushindi huo muhimu umeongeza matumaini ya Barcelona kutwaa ubingwa msimu huu, hasa baada ya mpinzani wao mkubwa, Real Madrid, kupoteza mchezo wao mapema siku hiyo.

Katika pambano hilo, Atletico Madrid walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Giuliano Simeone dakika za mwishoni mwa kipindi cha kwanza. Hata hivyo, Barcelona walijibu haraka kupitia kwa Marcus Rashford aliyesawazisha dakika chache kabla ya mapumziko.

Mchezo huo ulibadilika kwa kiasi kikubwa baada ya Atletico kubaki na wachezaji 10 kufuatia Nico González kupewa kadi nyekundu mwishoni mwa kipindi cha kwanza, jambo lililoipa Barcelona nafasi ya kutawala mchezo katika kipindi cha pili.

Licha ya upinzani mkali kutoka kwa Atletico, mshambuliaji nyota Robert Lewandowski aliifungia Barcelona bao la ushindi katika dakika za mwisho, akimalizia mpira uliorudi kutoka kwa kipa.

Matokeo hayo yanaifanya Barcelona kujitanua kileleni kwa tofauti ya pointi saba dhidi ya Real Madrid baada ya kufikisha alama 76, huku zikiwa zimebaki takribani mechi nane kumaliza msimu.

Mapema, Real Madrid walipata pigo baada ya kufungwa 2-1 na Mallorca, matokeo ambayo yamevuruga kwa kiasi kikubwa hesabu zao za kuwania ubingwa na kuipa Barcelona nafasi kubwa zaidi ya kunyakuwa taji la La Liga msimu huu.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE →
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
5h ago
READ MORE →
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE →
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE →
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
11h ago
READ MORE →
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE →
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE →
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE →
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
17h ago
READ MORE →
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE →