Local,Normal News,Simba, Yanga

SIMBA YAMKOMALIA DAMARO, YAPANGA KWENDA CAS NA FIFA

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 Apr 2026
SIMBA YAMKOMALIA DAMARO, YAPANGA KWENDA CAS NA FIFA

Klabu ya Simba SC imetangaza azma ya kupeleka shauri lake katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo,Court of Arbitration for Sport (CAS), kufuatia kutoridhishwa na uamuzi wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Tanzania Football Federation uliotupilia mbali kesi yao dhidi ya mchezaji Mohamed Damaro.

Hatua hiyo imetangazwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba,Crescentius Magori, aliyesema klabu hiyo imefanya tathmini ya kina na kubaini kuwa kuna dosari katika maamuzi yaliyotolewa na mamlaka husika.

Magori alisema mbali na kwenda CAS, Simba pia inapanga kuiandikia barua FIFA kupinga hatua ya kumpa uraia wa Tanzania mchezaji huyo, wakidai hana sifa za kuitumikia timu ya Taifa.

Alieleza kuwa suala hilo linaibua maswali kuhusu usawa wa kanuni katika uendeshaji wa soka nchini, akidai kuwa linaweza kuipa faida klabu moja kwa kuwa na wachezaji wa kigeni zaidi ya kiwango kinachoruhusiwa.

β€œKuhusu mchezaji Mohamed Damaro, tulikaa na kutafakari kwa kina, ni jambo ambalo halijakaa sawa. Ni kama kuna klabu moja inatumia nafasi hiyo kuwa na wachezaji wa kigeni zaidi ya walioruhusiwa kikanuni,” alisema Magori.

Aidha, alibainisha kuwa mwaka jana Simba iliwasilisha maombi ya kubadili uraia kwa baadhi ya wachezaji wake, lakini hadi sasa hayajajibiwa, jambo alilodai linaonyesha kukosekana kwa mizania sawa kwa klabu zote.

β€œMwaka jana na sisi tuliandika barua ya kubadili uraia wa wachezaji wetu lakini haijajibiwa hadi leo. Ligi ikiwa haina mizania sawa si jambo linalokubalika,” alisisitiza.

Magori aliongeza kuwa si sahihi kwa mchezaji kupewa uraia kwa lengo la kuchezea klabu pekee bila kuwa na uwezo wa kuitumikia timu ya Taifa.

β€œKama mtu anapewa uraia ili tu achezee klabu bila timu ya taifa si jambo linalokubalika. Damaro hata ipite miaka 100 hawezi kucheza timu ya Taifa,” alisema.

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
4m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
33m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’