Local,Normal News,Simba, Singida, Yanga

Imoro, Barker washinda tuzo za ligi kuu March 2026

Joel JJ By Joel JJ
β€’
8 Apr 2026
Imoro, Barker washinda tuzo za ligi kuu March 2026

Beki wa Singida Black Stars, Ibrahim Imoro amechaguliwa kuwa mchezaji Bora wa mwezi Machi wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2025/26, huku Steve Barkerwa Simba akichaguliwa Kocha Bora wa ligi hiyo kwa mwezi huo.

Imoro alionesha kiwango kizuri chenye mwendelezo kwa mwezi huo ikiwa ni pamoja na kufunga mabao matatu katika michezo mitano ambayo Singida ilicheza na kuisaidia timu yake kupanda kutoka nafasi ya 10 hadi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

Beki huyo aliwashinda Anicet Oura wa Simba na Lamine Jarjou wa Singida Black Stars alioingia nao fainali katika mchakato wa Tuzo za Mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kwa upande wa Barker aliyeingia fainali na Pedro Goncalves wa Yanga na David Ouma wa Singida Black Stars, aliongoza timu yake kushinda michezo miwili na kutoka sare miwili na kupanda kutoka nafasi ya tatu hadi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Wakati huohuo Meneja wa Uwanja wa Airtel mkoani Singida, Omar Malule, amechaguliwa kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Machi kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.

Katika hatua nyingine Omari Mponda wa Mbuni amechaguliwa Mchezaji Bora wa Mwezi Machi wa Ligi ya NBC Championship 2025/26, huku Zuberi Katwila wa Geita Gold, akichaguliwa Kocha Bora wa mwezi huo.

Mponda aliyeingia fainali na Yusuf Mhilu na Maulid Shaaban wote wa Geita Gold alionesha kiwango chenye mwendelezo ikiwa ni pamoja na kufunga mabao mawili kwa dakika 155 za michezo miwili aliyotumika mwezi huo.

Kwa upande wa Katwila aliyeingia fainali na Leonard Budeba wa Mbuni na Twaha Beimbaya wa B19, aliiwezesha timu yake kushinda michezo yote miwili iliyocheza na kupanda kutoka nafasi ya pili hadi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi.

Pia Kamati ya Tuzo imeteua magoli matatu bora ambayo yatapigiwa kura na mashabiki wa mpira wa miguu nchini, ili kupata Tuzo ya Goli Bora la Mashabiki kwa mwezi Machi.

Magoli hayo ni Prince Dube (Singida v Yanga dakika ya 38), Joseph Akandwanaho (TRA v Namungo dakika 90+1) na Ibrahim Imoro (Mbeya City v Singida Black Stars dakika ya 86).

Imetolewa na;
Idara ya Habari na Mawasiliano
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
Aprili 8, 2026

More Stories

Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
6h ago
READ MORE β†’
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
11h ago
READ MORE β†’
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
11h ago
READ MORE β†’
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
13h ago
READ MORE β†’
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
14h ago
READ MORE β†’
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
17h ago
READ MORE β†’
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
19h ago
READ MORE β†’
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
20h ago
READ MORE β†’
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
1d ago
READ MORE β†’
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
1d ago
READ MORE β†’