Local,Normal News,Yanga, TMA

Yanga yapania kuendeleza rekodi ya kibabe kombe la CRDB

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Apr 2026
Yanga yapania kuendeleza rekodi ya kibabe kombe la CRDB

Klabu ya Yanga imewataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa KMC Complex kesho Jumamosi, Aprili 11, kuipa sapoti timu hiyo itakapovaana na TMA Stars katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la CRDB.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe, alisema klabu hiyo inalenga kushinda mchezo huo ili kutinga hatua ya robo fainali na kuendeleza rekodi yao ya kutopoteza mechi katika mashindano hayo kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo.

β€œTuna miaka mitano sasa hatujapoteza mchezo kwenye Kombe la Shirikisho la CRDB. Ninaamini rekodi hii inakwenda kutuongezea nguvu ya kupambana katika mchezo dhidi ya TMA Stars,” alisema Kamwe.

Kamwe aliongeza kuwa mchezo huo utapigwa saa 12:30 jioni katika uwanja wa KMC Complex na akawataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao katika hatua hiyo muhimu ya mashindano.

β€œMuda wa mechi ni saa 12:30 jioni na itapigwa pale KMC Complex. Kwa mwanachama na shabiki wa Yanga huna sababu ya kukosa uwanjani kesho kwani mchezo ni wa hatua muhimu ya 16 bora,” alisema.

Akiendelea kuhamasisha, Kamwe alisisitiza umuhimu wa mashabiki kuwa sehemu ya timu, akisema mchezo huo unahitaji hamasa kubwa kutokana na ushindani wake.

β€œNjoo wewe, rafiki yako na familia yako mje mpate burudani. Hii si mechi ya kawaida kwa sababu ni hatua ya 16 bora. Tumeona Kombe la CRDB limetoa matokeo yasiyotarajiwa kwenye baadhi ya mechi,” alisema.

Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikilenga kusonga mbele na kuendeleza rekodi yao nzuri katika mashindano ya CRDB Federation Cup, huku wakitarajia changamoto kutoka kwa TMA Stars ambao nao wanaisaka rekodi ya kutinga robo fainali kwa mara ya kwanza.

More Stories

Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
4h ago
READ MORE β†’
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
8h ago
READ MORE β†’
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
9h ago
READ MORE β†’
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
11h ago
READ MORE β†’
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
11h ago
READ MORE β†’
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
17h ago
READ MORE β†’
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
18h ago
READ MORE β†’
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
1d ago
READ MORE β†’
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
1d ago
READ MORE β†’