Local,Transfer News,Yanga, Fenerbahce

Okello anukia ligi kuu ya Uturuki

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 May 2026
Okello anukia ligi kuu ya Uturuki

Maafisa wa klabu ya Uturuki, Fenerbahce S.K., wameripotiwa kuwepo nchini Tanzania kwa muda wa siku nne wakimfuatilia kiungo mshambuliaji wa Young Africans S.C, Allan Okello.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwanahabari wa Uganda, Ronnie Santos Mwine, wageni hao kutoka Uturuki wamevutiwa na kiwango cha mchezaji huyo wa kimataifa wa Uganda ambaye ameonyesha makali tangu ajiunge na Yanga katika dirisha dogo la usajili.

Okello ameanza maisha yake mapya kwa kishindo, akiwa tayari amechangia mabao matano na kutoa pasi za mabao saba kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, jambo lililomfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wanaofuatiliwa kwa karibu.

Inaelezwa kuwa maafisa wa Fenerbahce wanatarajiwa kuwepo uwanjani kesho wakati Yanga itakapovaana na Dodoma Jiji FC katika mchezo wa ligi utakaopigwa kwenye Uwanja wa Airtel Mtipa mkoani Singida.

Iwapo klabu hiyo ya Uturuki itaamua kumsajili Okello, itawalazimu kufungua mazungumzo rasmi na Yanga, ingawa hadi sasa hakuna mazungunzo yaliyoanza kati ya pande hizo mbili.

Okello alijiunga na Yanga akitokea Vipers SC ya Uganda, akisaini mkataba wa miaka miwili na nusu, na sasa anaendelea kuonyesha mchango mkubwa katika kikosi hicho cha Jangwani.

More Stories

Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
2h ago
READ MORE β†’
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
6h ago
READ MORE β†’
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
7h ago
READ MORE β†’
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
9h ago
READ MORE β†’
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
9h ago
READ MORE β†’
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
13h ago
READ MORE β†’
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
15h ago
READ MORE β†’
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
15h ago
READ MORE β†’
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
1d ago
READ MORE β†’
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
1d ago
READ MORE β†’