Timu ya taifa ya Ivory Coast imetangaza kikosi chake kitakachoshiriki Fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico, ikiwa na mchanganyiko wa wachezaji wenye uzoefu mkubwa barani Ulaya na vijana wanaochipukia.
Kocha Emerse Faé amechagua kikosi cha wachezaji 26, akilenga kuleta nguvu mpya, kasi na uimara katika kila idara ya timu.



