International,Normal News,Arsenal, Manchester City, EPL

Arteta na mbinu mpya za kubeba taji EPL msimu huu.

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
18 May 2026
Arteta na mbinu mpya za kubeba taji EPL msimu huu.

Mikel Arteta ameendelea kuonyesha namna anavyotumia mbinu za kipekee kuwajenga kisaikolojia wachezaji wa Arsenal, baada ya kuweka mfano wa kombe la Premier League katika uwanja wa mazoezi wa timu. Lakini kombe hilo lina tofauti moja kubwa, limeunganishwa na mfumo wa taa na linaweza kuwaka tu pale Arsenal watakapothibitishwa kuwa mabingwa.

Kwa siku zote za msimu, kombe hilo limekuwa pale mazoezini likiwa kimya, bila mwanga, kama ukumbusho wa kila siku kwa kikosi kwamba kazi bado haijakamilika. Wachezaji wamekuwa wakilipita kila wanapoingia mazoezini, wakilitazama kama lengo la mwisho ambalo bado hawajalifikia. Arteta ameonekana kutaka ndoto hiyo iwe mbele ya macho yao kila siku, si kwenye maneno pekee.

Hatua hiyo inakuja wakati Arsenal wako kileleni mwa msimamo wa ligi, wakiwa wamebakiza mechi mbili pekee kumaliza msimu ambazo ni dhidi ya Burnley wakiwa home na Crystal Palace wakiwa ugenini. Mbio za ubingwa bado ziko wazi huku Manchester City wakiendelea kufuatilia kwa karibu, lakini Arsenal wana nafasi nzuri ya kumaliza kazi na kubeba kombe hilo kwa mara ya kwanza mbele ya kikosi chao.

Mbinu za Arteta zimekuwa zikizungumziwa sana msimu huu. Mbali na kombe hilo, amewahi kutumia mbinu za kisaikolojia kama picha za mbwa wawindaji na hata njia nyingine za kuhamasisha kikosi kabla ya mechi kubwa. Ni njia zinazoonyesha jinsi anavyotaka wachezaji waishi ndoto hiyo kila siku, hadi ije kuwa ukweli.

Kwa wachezaji kama Bukayo Saka, Gabriel Martinelli na Kai Havertz, kombe hilo si mapambo tu. Limekuwa ishara ya kile wanachopigania. Kila mazoezi, kila jasho, kila mechi β€” macho yao yanarudi kwenye kitu kilekile: taji (Ubingwa)

Sasa Arsenal wako hatua mbili tu kutoka kutimiza ndoto hiyo. Kama watamaliza kazi yao, kombe hilo litawaka kwa mara ya kwanza β€” na kitendo hicho kinaweza kuwa picha moja itakayosimulia safari nzima ya msimu huu. Wakati mwingine, ishara ndogo hujenga historia kubwa

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
23h ago
READ MORE β†’