Local,Transfer News,Simba, Coastal

Winga Coastal Union kutua Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
6 Jun 2026
Winga Coastal Union kutua Simba

Klabu ya Simba SC imekamilisha mchakato wa kumsajili kiungo mshambuliaji chipukizi kutoka Coastal Union, Bakari Msimu, katika hatua ya kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao.

Taarifa zinaeleza kuwa usajili wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 umependekezwa moja kwa moja na kocha mkuu wa Simba, Steven Barker, ambaye amevutiwa na kasi na uwezo wa ubunifu wa kiungo huyo mshambuliaji.

Simba imeingia makubaliano ya mkataba wa miaka mitatu na mchezaji huyo, hatua inayoashiria imani kubwa ya klabu kwa kipaji chake na mipango ya kumkuza kwa muda mrefu ndani ya kikosi hicho cha Wekundu wa Msimbazi.

Msimu amekuwa mmoja wa wachezaji wanaofanya vizuri katika kikosi cha Coastal Union msimu huu, akijipatia umaarufu kutokana na uwezo wake wa kucheza kasi na ubunifu mkubwa.

Msimu anakuwa mchezaji wa nne wa ndani kusajiliwa na Simba mapema katika maandalizi ya kikosi kipya, akiwa ameungana na Nathaniel Chilambo, Ramadhan Chobwedo na Kelvin Nashon.

Uongozi wa Simba umeweka mkakati wa kukamilisha usajili mapema kabla ya dirisha rasmi kufunguliwa, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kujiandaa mapema na msimu wa mashindano 2026/27.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
37m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’