International,Normal News,Denmark, Tottenham, Manchester United

Eriksen kufanyiwa uchunguzi zaidi baada ya tukio la kuanguka tena uwanjani

Joel JJ By Joel JJ
8 Jun 2026
Eriksen kufanyiwa uchunguzi zaidi baada ya tukio la kuanguka tena uwanjani

Christian Eriksen amewekwa chini ya uangalizi wa karibu wa kitabibu baada ya tukio la ghafla lililotokea uwanjani ambapo alionekana kuanguka na kupoteza fahamu kwa muda mfupi kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Denmark dhidi ya Ukraine uliopigwa Jumapili usiku huko Denmark

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na timu ya matibabu, Eriksen alipata huduma ya haraka uwanjani na hali yake ilianza kuimarika baada ya muda mfupi, ambapo fahamu zake zilirejea.

Taarifa zinaeleza kuwa Eriksen anaendelea vizuri na hali yake kwa ujumla iko chini ya uangalizi wa wataalamu. Vifaa vya kudhibiti mapigo ya moyo vilivyowekwa mwilini mwake vimeonyesha kufanya kazi kama ilivyokusudiwa, na hakuna dalili za tatizo kubwa la haraka lililogunduliwa wakati wa tukio hilo.

Hata hivyo, madaktari wamesisitiza kuwa atafanyiwa vipimo zaidi hospitalini ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo la kupoteza fahamu ghafla.

“Sasa atafanyiwa uchunguzi zaidi hospitalini ili kubaini haswa kilichosababisha kutokea tukio hilo. Tunaendelea kuwasiliana naye pamoja na madaktari wake wa karibu hospitalini,” alisema daktari wa Denmark

Pia imeelezwa kuwa Eriksen mwenyewe amekuwa na hali nzuri ya mawasiliano baada ya tukio hilo na alituma salamu kwa wachezaji wenzake akiwahakikishia kuwa yuko sawa.

“Ila Christian anaendelea vizuri, na aliniomba nitume salamu zake kwa wachezaji wote na kuwaambia kwamba yuko sawa.”

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
5h ago
READ MORE →
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
8h ago
READ MORE →
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
10h ago
READ MORE →
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
12h ago
READ MORE →
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
14h ago
READ MORE →
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
15h ago
READ MORE →
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
15h ago
READ MORE →
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
17h ago
READ MORE →
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
20h ago
READ MORE →
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE →