Mamlaka za soka visiwani Zanzibar imefuta mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya timu ya Taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes' dhidi ya Uganda uliokuwa upigwe Alhamisi uwanja wa New Amaan Complex.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema leo, mchezo huo umefutwa kutokana na sababu za kiafya.
Ikumbukwe kwa sasa Uganda imekumbwa na janga la ugonjwa wa Ebola.





